
MSANII wa Bongo Muvi, Musa Kitale ‘Kitale’ amesema kuwa kwa upande wake anaona ni sawa tu kama kiki zikiendelea kutumika kwa sababu husaidia kukuza sanaa ya muziki.
Akizungumza na AMANI msanii huyo alisema kuwa siku zote katika mafanikio lazima kuwe na ushindani ambao unampa mtu hamasa ya kuendelea kujituma. Alisema kwa upande wake haoni ubaya wowote kwa msanii kufanya tukio la kuvuta hisia za wengi kisha akaachia ngoma yake.

Alisema jambo la msingi, ni kwamba msanii huyo azingatie kufanya kiki zenye kujenga na si kubomoa.“Binafsi naona suala la kiki liendelee tu kuwepo kwa sababu zinasaidia kukuza sanaa yetu, siku hizi kila mtu yuko bize na maisha yake hana muda wa kuingia YouTube na kuanza kuangalia kazi mbalimbali za wasanii.
‘Lakini kama msanii akifanya kiki kisha baadae ndio aje aachie wimbo wake lazima watu watapata hamasa ya kuangalia uko vipi, kwa hiyo kiki inasaidia kuwaweka mashabiki zetu ‘attention’ ila ushauri wangu wasanii wafanye kiki zenye kujenga na sio kubomoa,” alisema Kitale.
STORI; KHADIJA BAKARI NA MEMORISE RICHARD