
Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akiendelea na ziara yake Mkoani Mwanza leo Aprili 25, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaweka ndani (Mahabusu) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mjini Mwanza (MWAWASA), meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini Mkoa wa Mwanza (RUWASA), Meneja wa Maji Vijijini Wilaya ya Sengerema, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Sengerema na Mkandarasi.
Aweso ameagiza Watu hao wawekwe ndani hadi kesho atakapokutana nao ofisi ya RC Mwanza kwa maamuzi zaidi.
Amefikia maamuzi hayo baada ya kukutana na changamoto kubwa ya kutokamilika, kutumia pesa kinyume na BOQ utekelezaji usiokidhi vigezo kwa mradi wa maji tegemezi kwa Wilaya ya Sengerema wa Busurwangiri ukiwa umetumia Tsh. Bilion 1.8 na Wananchi hawapati maji hivyo kupelekea kunywa maji ya mashimoni yenye tope.