×

Wawili Wafikishwa Kortini kwa Tuhuma za Mauaji

Watu wawili wakazi wa Msakuzi Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji.

 

Washitakiwa hao ni Victoria Mseka na Mawazo Hassan wamesomewa shitaka linalowakabili na wakili wa Serikali Benson Mwaitenda mbele ya Hakimu mkazi Mahakama hiyo, Happy Kikoga.

Akiwasomea shitaka hilo wakili wa Mwaitenda amedai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 26, 2021 katika eneo la Msakuzi Wilayani Ubungo Dar es Salaam ambapo wanadaiw kumua Sauda Likiwa nakumtupa kinyume na makosa ya jinai kufungu cha 196 na 197 ya sheria ya mwaka 2019.

 

Wakili Mwaitenda amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

 

Awali kabla ya washitakiwa kusomewa shitaka lao hawakuruhusiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na Mamlaka ya kusikiliza Kesi za mauaji. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 6 mwaka huu.

Leave a Comment