×

Rais Samia Atumbua Watatu

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa viongozi watatu akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Profesa Tadeo Satta, Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Posta, Harun Kondo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa, inaeleza kuwa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga, inaeleza kuwa pia Rais Samia ametengua uteuzi wa wajumbe 6 wa Bodi ya TASAC pamoja na kuvunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

Taarifa hiyo inazidi kueleza kuwa uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo utafanywa baadaye.

Leave a Comment