×

Ninja Atamba Nileteeni Huyo Morrison

Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema amekuwa akizisikia kelele za mashabiki wa Simba wakitamba kwamba hatoweza kumdhibiti winga wa timu hiyo, Bernard Morrison katika mchezo wa watani wa jadi utakaochezwa Jumamosi hii.

 

Ninja ambaye kwa siku za karibuni amekuwa na namba ya uhakika kwenye kikosi cha Yanga, amesema kama aliweza kuwaficha Meddie Kagere na Chris Mugalu, basi Morrison aje tu kwani dawa yake atakuwa nayo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ninja alisema hawezi kuwa na presha kutokana na kile ambacho mashabiki wa Simba wanazungumza kwani yeye amejipanga kucheza na yeyote atakayepangwa naye.“Hayo ni maneno ya mashabiki hayawezi kunipa presha au kukaa kumuwaza huyo Morrison anacheza vipi.

 

“Nakubali kwamba ni mchezaji mzuri kwa sababu anajua nini ambacho anakifanya hasa akiwa na mpira, lakini kwangu nitajua namna ya kuweza kucheza naye. Aje tu.

 

“Kila unapoenda kwenye mechi lazima uwajue wapinzani wako unaokabiliana nao ili ujue nini cha kufanya kuwadhibiti, sasa hao mashabiki hayo ni maneno yao, siwezi kuogopa maana kumbukumbu za Fainali ya Kombe la Mapinduzi wanazo, alianza Kagere halafu akaja Mugalu, wote hawakuweza kufunga, na huyo wakimleta basi nitajua cha kumfanya, kikubwa tuombe uzima siku ifike,” alisema Ninja.

STORI NA IBRAHIM MUSSA

Leave a Comment