
MKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva, Juma Nature amefanya maajabu katika Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar baada ya kuingia jukwaani na kuwakubusha mashabiki wake kwa kupiga nyimbo zake zote kali kuanzia Sonia, Kighetogheto na nyingine kibao.

Shoo hiyo ni maalum kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid Al-Fitr ambapo msanii mkali wa Bongo Fleva kutoka WCB, Zuchu anatarajiwa kuangusha Bonge la Shoo usiku huu wa kuamkia Jumamosi, Mei 15, 2021.