×

🔴#LIVE: Rais Samia Awaapisha Majaji Wapya

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, leo Jumatatu, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam. Majaji hao aliwateua hivi karibuni.

 

Akizungumza wakati akitoa hotuba yake mara baada ya kuapisha alisema;Ā “Nianze kwa usemi wenu unaosema haki iliyochelewa ni sawa na haki iliyonyimwa, tatizo la ucheleweshwaji wa kesi nchini lipo na mara kadhaa nimekuwa nikimsikia Jaji Mkuu akisema linachangiwa na upungufu wa Majaji ni imani yangu tatizo litapungua.

 

“Kati ya Majaji 7 wa Mahakama ya Rufaa walioapa leo 3 ni wanawake na katika 21 wa Mahakama Kuu 10 ni wanawake, sikuchagua kwa uanamke wenu tulipima uwezo wenu, ombi langu mkajiamini najua wanawake wakikaa Mahakamani ni wazuri zaidi kuliko wanaume.

 

“Nawaombeni mkaongoze vyema, lakini mkaongozwe vyema na imani, utu na nafsi zenu sasa nafsi ikiwaelekeza kwenda kuchukua fedha na kunyima haki ya mwingine kumpa mwingine ujue umeshatetereka na tukikugundua itakuwa umekosa zile sifa zilizokupandisha,” amesema Rais Samia.

 

Leave a Comment