
MAJESHI ya kulinda amani yamethibitika kuwa silaha bora zaidi ya Umoja wa Mataifa katika kuzisaidia nchi kadhaa kutoka katika matatizo na kuingia katika anga la amani.
Majeshi hayo yana nguvu ya kipekee, ikiwa ni pamoja na uhalali, kubeba majukumu pamoja na uwezo wa kupeleka majeshi au polisi sehemu mbalimbali duniani na kuyajumuisha na makundi ya kiraia katika kulinda amani.
Jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha amani huwaunganisha walimwengu kupitia Baraza Kuu la Umoja huo, Baraza la Usalama, Sekretariati yake, katika kutoa majeshi na polisi kwa serikali zinazohitaji msaada huo ili kujenga amani na usalama duniani.
Nguvu ya yote haya hutokana na Azimio la Umoja wa Mataifa na nchi zote ambazo hushiriki katika kutoa utajiri na nguvu mbalimbali kwa ajili ya lengo hilo.