
NAIBU Waziri wa Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda wamezindua Ushirika wa Wavuvi katika Kisiwa cha Zilagula.
Ushirika huo ulipata mkopo wa shilingi million 10.7 ziliwawezesha kutengeneza mitumbwi mikubwa sita.

Sambamba na kuzindua ushirika huo, viongozibhao wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya wavuvi katika kisiwa hicho.

Naibu Waziri Ulega amewapongeza wanaushirika hao huku akiwataka kuimarisha ushirika huo na kuwahakikishia kuwa serikali ipo tayari kutoa fedha kwa watu ambao wapo kwenye vikundi ili wajiendeleze.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Eric Shigongo amesema nia yake ni kuona wananchi wote wa Buchosa wanafanikiwa kiuchumi na kutatua changamoto zinazowakabili huku akiwasihi kujituma katika kuchapa kazi maana ndio njia pekee ya kuwakwamua kiuchumi, kujiletea maendeleo na kuliletea maendeleo Taifa.