×

RC Songwe Agawa Miche Ya Michikichi Kwa Wakulima

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omary Mgumba akimkabidhi mwananchi mche wa mchikichi kwa ajili ya kwenda kuupanda shambani kwake.
Mgumba na viongozi wengine wakiangalia miche ya michikichi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba (katikati) akiendelea kukabidhi miche ya michikichi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba (katikati) akiendelea kukabidhi miche ya michikichi.
…Akiondoka eneo la tukio.
Mmoja wa viongozi aliokuwa ameambatana nao akizungumza jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omary mgumba amewagawia wakulima wa wilya ya Mbozi na Momba mkoani Songwe pamoja na wilaya ya Bosokelo na Kyela Miche ya michikichi bure ili kuongeza uzalishaji wa mbegu za Michikichi kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula nchini.
Hafla hiyo imefanyika leo May 29, 2021 katika kijiji cha Magamba wilayani Mbozi mkoani Songwe. Mhe Mgunba amegawa miche hiyo iliyokuwa katika kitalu cha Michikichi iliyooteshwa na kukuzwa na Wakala Wa Mbegu wa Selikali ASA katika shamaba lao kubwa la mbegu lenye ukubwa wa ekari 4876 lililopo Magamba Mbozi.
Baada ya hafla ya uzinduzi wa ugawaji miche kwa wakulima mkuu wa mkoa huyo aliendelea na ziara yake ya Kutembelea wilaya zake za Mkoani Songwe ambapo leo alitegemea kuwa katika Wilaya ya mbozi baada ya kutembelea wilaya za Momba na Songwe ambapo ziara hizo ni kujitambulisha katika eneo lake la kazi na kukagua shughuli za maendeleo zinazofanyika katika mkoa wake.

Leave a Comment