×

Mzee Abdul Atoa Tamko Zito Kuhusu Diamond “Damu Yangu”- Video

MZEE Abdul Juma ambaye amekuwa akifahamika kama baba mzazi wa Diamond Platinumz amesema hawezi kumlaumu Diamond, kwani tangu alipotoka Hospitali, jina, kadi ya kliniki, ofisi na kila kitu vimeandikwa majina yake lakini Mama Diamond ameamua kusema si mtoto wake.

 

Mzee abdul amefunguka hayo kupitia kipindi cha HotPot kinachoruka kupitia Global Radio na kuongeza kuwa Mama Diamond amemchanganya mwanaye kwa sababu ukweli anaujua lakini hakutaka kusema kwamba baba yake ni nani.

 

“Unakuja kuwa mkubwa unaambiwa baba yako ni mwingine, ndio maana hajaongea kwa sababu mama kamchanganya hata yeye. Jina la Mzee Nyange nimekuja kulisikia mwisho kabisa, nilikuwa sijui na hata simjui, ndio maana nikakasirika nikasema asitumie tena jina langu atafute kaburi la baba yake.

 

“Mimi nimekunjua roho, nilitumia hasira kwa sasa nimesamehe atumie tu jina langu kwa sababu nimezoeleka naitwa Baba Diamond, Babu Tiffah, hata zamani alipokuwa akilitumia nilikuwa sifaidiki kwa chochote, nimemsamehe bure.

 

“Kiukweli ishu ya Diamond kunikataa iliniumiza sana, nimekaa ndani kwa miezi miwili bila kutoka wala kufanya shughuli zangu, ukitoka tu unanyoshewa kidole ‘huyoo’ mpaka msiba wa Rais Magufuli ulipotokea ndipo sakata lile likazima.

“Siku ya Eid nilikuwa nimelala nikaona mzigo umeingia kwenye simu, nikapigiwa simu nikauliza wewe nani? akasema mimi Naseeb nikauliza Naseeb nani? Mimi mwanao. Nilishukuru nikasema hii kweli damu yangu, mimi na Diamond maisha yanaendelea.

“Baada ya Diamond kunitumia pesa nikaita mashehe na majirani nikatia ubani pale nikafanya dua, watu wakala chakula cha asubuhi, baada ya muda Queen darleen naye akatuma, nilikuwa na Baraka.

“Mpaka sasa sijajua mama Diamond ni kitu gani kilimpata, au wapi nilimboa mpaka akaamua kusema hivyo, au labda amechanganyikiwa na kipato, haamini kama hela hizo wangepata, sijaelewa. Kama tatizo ni hivyo kwa nini wasingeniambia zamani, ningekuwa najua tangu zamani ningeenda kwenye shughuli zao wananialika kumbe wanani-enjoy?

“Kabla ya lile tukio Mama Naseeb nilikuwa naongea nae vizuri sana kiutu kabisa, mpaka mwenzangu Shamte akawa anasema uje kuwaona wajukuu zako bwana, lakini shida ilitokea Zari alipofiwa akaenda kwao Uganda, ndipo ratiba ikaborongeka.

“Inaniumiza, mwenzangu anaishi maisha mazuri yanayotokana na matunda ya mtoto ambayo nimeshiriki katika malezi yake, lakini siwezi kuingilia. Unaweza kuwa polisi una ndugu ana kesi lakini mkubwa wako wa kazi akakwambia huyu hawezi kutoka sababu kesi yake ni kubwa.

“Diamond alipiga nyimbo zake zote akapiga ngoma yangu ya ‘Dudu la Yuyu’, alipopiga ile ‘Shang’anda’ Waarabu wote wakanyanyuka.

 

“Siwezi kumpangia Diamond amuoe nani, mimi ni mzazi yeyote atakayeletwa mimi sina shida, yeye ndo anajua anataka mwanamke wa aina gani. Ameshasema sana kuwa anataka kuoa lakini haoi, hiyo ni nyimbo.

“Queen Darleen ypo pale Wasafi kama mfanyakazi, akiambiwa, hakutegemea kama yatakuwa hayo. Mungu ndio anajua utakuwa wapi wakati gani, Mungu anaweza akakushusha.

“Mara ya mwisho Hamisa Mobetto nilikuwa nawasiliana naye vizuri lakini naona siku hizi naye kanipotezea, ukimpigia simu anabadilisha sauti ‘wewe nani?’, Babu Tiffah, anakata, ikaniuma sana lakini nikasema hakuna shida, nadhani anahisi nitampiga bomu.

“Mimi namtakia Mama Diamond maisha marefu, waishi vizuri na Anko Shamte, Mungu awajalie wapate mtoto, siku zikifika tuzikane, hamna kingine zaidi ya kuzikana,” amesema Mzee Abdul.

 

Leave a Comment