×

Mondi Amzawaida Gari Mkubwa Fela

 

Msanii wa maarufu wa Bongofleva, Naseeb Abdul amemzawadia gari aina ya Honda CRV mmoja wa mameneja wake, Saidi Fella ‘Mkubwa Fela’ ikiwa ni zawadi katika kutimiza miaka 23 ya ndoa yake.

Fela ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule – CCM alisema Mondi ameona umuhimu wa meneja wake kuhama kutoka kwenye Prado ambayo ameitumia kwa muda mrefu kiasi cha watu kumshangaa.

“Mondi hajawahi kuniambia kama ana mpango wa kuninunulia gari lakini juzi nashangaa nimeletewa gari na mwanangu mmoja anaitwa Mudi akaniambia bana Naseeb kasema nikuletee… nikamuuliza kweli, ningekuwa mtoto ningelia vilevile kwa furaha lakini sisi wakubwa mambo ya magari ni jambo la kawaida.

“Kawa hiyo nashukuru kwamba ameona nini nimefanya kitu kwake kwa miaka zaidi ya 10 akaniambia bwana nakupongeza, nilipompigia simu alianza kuniambia kwanza nakupongeza licha ya kwamba umenilazimisha nioe lakini pili nimependa wewe na wife wako sasa umetimiza zaidi ya miaka 20 ya ndoa kwa hiyo nakupongeza,” alisema.

Aidha, Fela alisema ameipenda gari hiyo kwa sababu mjini zipo gari za aina hiyo chache kama tano au sita.

CC: @mushigabriel.

Leave a Comment