
RAIA mmoja wa China mwenye umri wa miaka 41 amethibitishwa kuwa na kisa cha kwanza cha maambukizi ya homa ya ndege baada ya kubatiwa matibabu
Maafisa hawakutoa maelezo kuhusu jinsi mtu huyo alivyoambukizwa virusi hivyo vya H10N3 ambavyo vinadaiwa kusambaa kwa urahisi miongoni mwa wanadamu.
Tume ya afya mjini Bejing NHC imesema siku ya Jumanne kwamba mkaazi huyo wa mji wa Zhenjiang alilazwa hospitali tarehe 28 mwezi Aprili na kupatikana na virusi vya H10N3 mwezi Mei 28.
“Hakuna hata kisa kimoja cha ugonjwa huo kilichoripotiwa duniani, Kisa hiki ni cha maambukizi kutoka kwa ndege hadi kwa binadamu , na hatari ya kusambaa kwake ipo chini sana ”, ilisema tume hiyo, kulingana na ripoti ya gazeti la Global Times.
Tume hiyo pia ilisema kwamba virusi hivyo haviwezi kuhatarisha maisha ya ndege na kwamba pia haviwezi kusambaa kwa haraka.
Shirika la Afya duniani WHO liliambia Reuters kwamba wakati huu hakuna ishara ya maambukizi ya kutoka binadamu mmoja hadi mwengine.