
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kuingizwa kwa shilingi milioni 500 katika kila Jimbo ili kufanikisha ujenzi wa barabara kupitia TARURA.
Mgawanyo huo unatokana na uamuzi wa Rais Samia kuidhinisha shilingi bilioni 172 kwa ajili ya kuboresha miradi ya barabara inayosimamiwa na TARURA.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa TAMISEMI, @ummymwalimu amesema; “Kwa mara ya kwanza tumepata fedha bilioni 172 kutoka mfuko mkuu wa hazina kwa sababu fedha hizi tumezipata harakaharaka na bajeti ilishapitishwa na Kamati, tumetumia maamuzi ya jumla kila jimbo tunapeleka milioni 500 kwa ajili ya TARURA ili barabara zijengwe.
“Na hii ndiyo kazi mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesikia kilio chenu.”
Hatua ya utengenezaji wa barabara katika kila jimbo ni muendelezo wa Rais Samia kuhakikisha kila kona ya nchi inakuwa na barabara za uhakika ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa shughuli za kiuchumi.