×

Zari Atua Bungeni Dodoma – Video

Mama Watoto wa Mwimbaji Diamond Platnumz , zarithebosslady ni miongoni mwa Wageni waliokaribishwa Bungeni Dodoma leo kushuhudia shughuli mbalimbali za Bunge kwa mwaliko wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Damas Ndumbaro, Zari kwa sasa ni Balozi wa Hiari wa Utalii Tanzania.

Zari alitua Airport Dar es salaam juzi akitokea South Africa kwa ajili ya kazi zake za Ubalozi ikiwemo kugawa taulo za kike kwa Wasichana mbalimbali Dar es Salaam.

Wengine waliokaribishwa Bungeni leo ni Msemaji wa Simba SC, Hajia Manara na mkewe Naheeda, pamoja na mwanamuziki AY.

Leave a Comment