
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Argentina Mauro Icardi na mke wake Wanda Nara Icardi wametembelea Tanzania kwa ajili ya utalii.
Icardi anakuwa Staa wa pili wa soka kutembelea Tanzania katika kipindi cha mwezi June 2021 baada ya Mamadou Sakho na Mke wake Majda Sakho.
Kamishna msaidizi mwandamizi mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete amesema kuwa Mwanamichezo huyo wa Timu ya Taifa Argentina amefika nchini na mkewe ambaye pia ni wakala wake kwenye masuala ya mpira.