
TIMU ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mkali, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, imemkali kooni Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Hatua hii imekuja baada ya Lebo ya Kings Music iliyo chini ya Kiba kutumia ukurasa wake kwenye mitandao ya kijamii na kuweka posti ambayo inadaiwa ilimlenga Diamond au Mondi.
Inafahamika kwamba, Mondi amekuwa akitumia ‘hashtag’ ya SwahiliNation, jambo ambalo Kings Music wameingilia kati na kutoa maana halisi ya hashtag hiyo.

Kwa mujibu wa Team Kiba, hashtag hiyo inamfaa Kiba ambaye ndiye mtu mwenye maana halisi ya hashtag hiyo ya SwahiliNation.
Kupitia ukurasa rasmi wa Kings Music wameandika;“True SwahiliNation ni fact, hajabebwa na international collabo, hajatumia Nigeria Fleva wala Amapiano, hajatumia vionjo vya America, hana janjajanja, hafanyi kiki, hatii huruma zaidi ya kusimama na muziki wake na mashabiki wake na wala hatumii nguvu kubwa kupushi kazi zake, lakini anashinda matuzo ya kimataifa na anafanya mashoo ya kimataifa, halafu yupo on top kwenye game miaka 18 sasa hajawahi kushuka wala kuchuja ndiyo maana anaitwa mfalme wa muziki Africa…
”Baada ya posti hiyo ndipo mashabiki au Team Wasafi wakaibuka na kumshambulia Kiba kwamba, huwa anatumia mgogo wa Mondi ili kupata kiki hasa pale anapoelekea kusahahulika.
Baada ya hali kuwa, mbaya huko maoni mengi yakiwa ‘machafu’ ndipo lebo hiyo wakaondoa bango hilo kwenye kurasa zao na kutuliza upepo.Ishu hiyo imekuja siku chache baada ya lile sakata la Salada lililotolewa na Kiba ambalo wengi walilihusisha na Mondi pia.
Stori; Mwandishi Wetu, Dar