×

Mume wa Amber Ruty Akana Kujichubua

MUME wa Msanii wa Bongofleva, Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Rutty’, Said Bakary amesema si kweli kwamba anajichubua kama watu wanavyodai.

 

Said ambaye pia naye ni msanii, alisema watu wanaosema amejichubua ni wale ambao hawamfahamu kwa undani.

 

 

Akipiga stori na 255global radio jana Juni 6, 2021 jijini Dar alisema inawezekana ni kweli rangi yake imebadilika na kuwa mweupe ila ni kutokana na hali ya maisha mazuri anayoishi sasa.

 

 

Alisema hapo awali ambapo alikuwa kinyozi, maisha yalikuwa ymemgonga kiasi cha kutembea juani kila mara ndio maana rangi ya ngozi yake ikawa nyeusi ila sasa kwa kuwa amepunguza kutembea juani na anakula kivulini rangi yake aliyozaliwa nayo imerejea.

Leave a Comment