Prof.Ndalichako Akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia
Global Publishers June 7, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anaesimamia Ukanda wa Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.Kikao kikiendelea.Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anaesimamia Ukanda wa Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo, Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe na Viongozi wengine wa Wizara mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika jijini Dodoma.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu mara baada ya kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anaesimamia Ukanda wa Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, leo Juni 7, 2021 Jijini Dodoma amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dkt Taufila Nyamadzabo kuzungumzia utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu pia amehudhuri kikao hicho.
Baadhi ya miradi iliyojadiliwa ni Mradi mpya wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambao unalenga katika kuimarisha Elimu ya Sekondari nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza nafasi zaidi kwa kujenga shule zaidi ya 1000, maendeleo ya Mradi wa EP4R, miradi inayolenga kuboresha Elimu ya Juu Nchini ikiwemo Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) na Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ).