×

Tanzia: Mwanasiasa Mkongwe Mizindakaya Afariki Dunia

MWANASIASA mkongwe nchini Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya amefariki dunia leo  jioni Juni 7, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mkoani Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika uhai wake, Dkt. Mzindakaya amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ukuu wa mkoa na mbunge wa jimbo la Kwela mkoani Rukwa kwa takribani miaka 45.

Mtoto wa Marehemu, Paul Mzindakaya amethibitisha kifo cha baba yake.

 

Leave a Comment