
Mwili wa mwanasiasa mkongwe, Dk. Chrisant Mzindakaya aliyefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa, unatarajiwa kuzikwa Alhamisi Juni 10, 2021 wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Msemaji wa familia, Frank Mzindakaya amesema ibada ya mazishi itafanyika kesho katika kanisa lililopo Hospitali ya Muhimbili kisha mwili utasafirishwa kwa ndege kwenda Sumbawanga kwa maziko yatakayofanyika Alhamisi.
Msemaji huyo ameongeza kuwa kabla Mzindakaya hajafariki, alitoa maelekezo ya mahali anapotaka azikwe akifa, hivyo familia itatekeleza jambo hilo na kwamba maandalizi yanaendelea.