Rais wa Botswana Dr. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi ameondoka hii leo baada ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambapo amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikianano wa afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Akizungumza mara baada ya kuagana na Rais wa Botwana, Balozi Mulamula amesema ziara hiyo ilikuwa na mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kudumisha mahusiano baina ya nchi hizo.
Akizungumza kuhusiana na watanzania kuwekeza nchini Botswana Balozi Mulamula anafafanua. Ziara hiyo ya Rais huyo wa Botswana ni uendelezaji wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Botswana na na kuendeleza Diplomasia ya kiuchumi kati ya nchi nyingine.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx