×

Mwalimu Achomwa Msumari Kichwani na Mwanafunzi

MAKACHERO wa kaunti ya Kericho nchini Kenya wanamsaka mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyemshambulia mwalimu mkuu wake kwa kumchoma msumari kichwani.

 

Mwanafunzi huyo ni wa shule ya upili ya Ainamoi na alimshambulia mwalimu mkuu baada ya kutakiwa kulipa karo.

 

Kwa mujibu wa  ripoti ya polisi, mwalimu mkuu alimtaka mwanafunzi huyo kulipa karo ya KSh 7000 lakini akaamua kuendelea msumari na kumchoma kichwani.

 

Kisa hicho kimezua wasiwasi katika shule ya upili ya Ainamoi kaunti ya Kericho huku kikosi cha waalimu kimesema kinahofia maisha yao na sasa wanataka serikali na wazazi kuwahakikishia usalama

 

Mwalimu huyo wa kiume alifikishwa hospitali kupata matibabu na hali yake imeelezwa kuwa salama sasa.

 

Picha za mwalimu huyo akivuja damu kichwani baada ya msumari huo wa inchi nne kumuingia kichwani.

 

Kisa hicho kimeipingwa na kuibua mjadala mkubwa mkali na wazazi eneo hilo huku kwenye mitandao ya kijamii wakihoji kuhusu kizazi cha sasa cha wanafunzi.

 

Leave a Comment