
ALMASI inayoaminika kuwa ya tatu kwa ukubwa kuwahi kupatikana imewekwa kwenye maonesho nchini Botswana, jiwe hilo la thamani – lenye uzito wa karati 1,098 – lilioneshwa Rais Mokgweetsi Masisi, baada ya kampuni ya Almasi, Debswana, kuipata.
Jiwe hilo ni zito kidogo kuliko almasi ya pili ya ukubwa duniani ambayo pia ilipatikana Botswana mwaka 2015, Botswana ndio mzalishaji mkubwa wa madini ya almasi Afrika.
Debswana ni mshirika wa pamoja kati ya serikali na kampuni kubwa ya madini ya almasi duniani De Beers na hadi asilimia 80 ya kipato kinachotokana na mauzo hayo huelekezwa kwa hazina ya serikali kupitia pesa zinazolipwa kama faida, mrabaha na kodi.
Waziri wa madini nchini Botswana, Lefoko Moagi, amesema ugunduzi huo wa hivi karibuni umewasili wakati muafaka baada ya janga la virusi vya corona lililokumba Botswana kusababisha kupungua kwa mauzo ya almasi mwaka jana.