

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh21.8 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana
ambalo lilikuwa Sh15.25 bilioni.
Akipokea mfano wa hundi, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwamwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchimajirani.
Dk Mpango alisema kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazimawaongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.Gawio lililotolewa jana ni sehemu ya faida ya Sh206 bilioni ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa
kuishia desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.
Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayokwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.
Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya lakini nataka muongeze ubunifu ilimwaka muwe zaidi ya hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazinzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa," amesema Dk Mpango.
Kuhusu NMB aliwataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu ribakubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.
Aliwataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathiminivinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kamakumejaa.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NMB Edwin Mhede alisema tayari fedha hizo zilishawekwakatika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana namwenendo wavyoona.
Mhede alitaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katikakuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.
Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa Serikalini Sh245bilioni kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya Sh2 bilioni kwenyehuduma za kijamii.
Bi. Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh1.1 trilioni kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwaviwango vinavyotakiwa.