
Kwa wapenzi wa Rege jina la Bunny Wailer siyo geni kwani wanakumbuka nyimbo zake kama
Redemption Song, Rise and Shine, Is This Love na nyingine kibao.
Basi bana, Wailer ambaye ni raia wa Jamaica, alifariki dunia Machi 2, mwaka huu, lakini mwili wake
ulizuiliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa kukosa hati ya mazishi kufuatia deni kubwa la bili ya
matibabu.
Mazishi ya Wailer ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 yalifanyika jana, Ijumaa kwenye
hafla iliyohudhuriwa na familia pekee kufuatia mikakati iliyowekwa na Serikali ya Jamaica kudhibiti Virusi
vya Corona.
Hata hivyo, hafla hiyo ambayo ilifanyika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Dreamland nchini Jamaica
ilioneshwa kwenye mitandao ya kijamii.
Wailer alikuwa mwanzilishi pekee wa Kundi la Wailers aliyekuwa amebaki baada ya waanziishi wengine,
Bob Marley na Peter Tosh kuaga dunia mwaka wa 1981 na 1987.
Mwili wa marehemu umekuwa umezuiliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa kukosa hati ya
mazishi kufuatia deni kubwa la bili ya hospitali.
Inadaiwa kuwa familia ya marehemu ilikuwa na mzozo na kampuni ya kutengeneza muziki iliyowatataka
kutia saini mkataba ili waweze kulipa deni la hospitali.
Watoto wa marehemu waliweza kulipa deni ya hospitali karibia mwisho wa mwezi Aprili na kuanza
shughuli za mazishi.
STORI NA SIFAEL PAUL | GPL