
MEYA Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto ameshiriki katika Mahafali ya pili katika Chuo cha Ufundi APEC kilichopo katika Kata ya Kivule Jijini Dar es salaam. Katika Mahafali hiyo Mgeni Rasmi alikuwa SACP Wilfred Mutafumngwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania.
Kumbilamoto amewapongeza wahimu wote walio hitimu mafunzo ya Ufundi katika Chuo hicho na kuwata kuendelea kutumia vyema Mafunzo walio yapata ili yaweze kuwasaidia katika maisha yao hasa kwenye Ujasiriamali wa kujiari.

Aidha amewapongeza viongozi wote pamoja na Walimu kwa kazi nzuri ya kwa kuendelea kutoa mafunzo ambayo wamekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi katika Kata ya Kivule na meneo ya jirani.

Kwa upande wa Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani SACP Mutafungwa amewasisitiza Wahitimu kuendelea kuwa mabarozi kwa jamii katika kusimamia sheria za usalama barabarani ili kuendelea kuepusha ajari za barabarani.
Mwisho uongozi wa Chuo cha APEC uliwatunuku vyeti Wahitimu wote pamoja Wahitimu walio fanya vizuri kwa upande wa taaluma, Lakini pia uongozi wa Chuo ulitoa vyeti vya pongezi na Shukrani kwa Mgeni Rasmi, Meya wa Jiji la Dar es salaam pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kwa kazi nzuri wanazozifanya.