×

Backstreet Boy’s Wamerejea?

WAHENGA mpoo!, basi lile kundi maarufu la muziki wa Pop na Rnb, Backstreet Boys umeambiwa linajifua kurejea tena kwenye game baada ya kutikisa kuanzia miaka ya 90.

Kundi hilo lililoanzishwa huko mjini Orlando, Florida nchini Marekani mwaka 1993, liliwaunganisha waimbaji wakali kama vile A. J. McLean, Howie Dorough, Brian Littrell, Nick Carter na Kevin Richardson.

 

Sauti zao tamu zilifyatua vibao vikali kama vile ‘as long as you love me’, vilivyokuwa vikinogesha dedication katika barua za mahaba.

 

Unaambiwa wakali hao wanajifua kusaka style mbalimbali za kuwaburudisha mashabiki wa mziki huo kama wanavyoonekana hapa.

Story: Mushi Gabriel

Leave a Comment