
Ofisi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imetangaza orodha ya majina ya ajira kwa kada ya afya kuona majina hayo bonyeza hapa
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ametangaza ajira za Elimu 6,749 kwa shule za Msingi na Sekondari na Wataalamu wa Afya 2,726.
Akitoa Taarifa hiyo Jijini Dodoma mapema leo hii Prof. Shemdoe amesema waombaji wa kada ya Ualimu walikua 99,583 na Wataalam 37,437 wa kada ya afya, wakiwemo wenye ulemavu 1,099 waliomba nafasi hizo.
“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi Walimu 6,949 (3,949 wa shule za Msingi na 3000 wa shule za sekondari) na Wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi” amesema Prof. Shemdoe.
Ametaja vigezo vilivyotumika kuwapata watumishi waliokidhi sifa kuwa ni pamoja na Mwaka wa kuhitimu chuo ambapo waombaji waliomaliza mapema zaidi (mwaka 2012 hadi 2019) kulingana na mahitaji yaliyopo katika kada husika wamepewa kipaumbele.