×

Rais Samia: Taifa Limepoteza Mhandisi Mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyekuwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kuwa ni Mhandisi Mahiri na Mzalendo wa kweli na kwamba Daima alikuwa tayari kuitumikia nchi yake kwa moyo wake wote.

 

Ameyaseama hayo leo Julai 2, wakati alipoongoza zoezi la kuaga mwili wa mhandisi Mfugale kwenye viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.

 

“Mhandisi Mfugale ameaga dunia Juni 29 baada ya kuugua kwa muda mfupi, kifo hiki kimeacha simanzi na pengo kubwa katika familia na serikali, familia imepoteza mtu muhimu waliyempenda, Taifa limepoteza Mhandisi mahiri na mzalendo wa kweli”

 

Aidha Rais Samia Ameongeza kuwa Mara ya mwisho kuonana na Mhandisi Patrick Mfugale, ilikuwa kwenye daraja la JPM pale Busisi, Mwanza, akiwa mzima na makini.

 

“Kwa niaba ya serikali nitumie fursa hii kutoa pole kwa mke wa marehemu Mfugale, watoto wake, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu naelewa machungu yenu ni makubwa mno lakini yote haya ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu”

 

Kwa mujibu wa ratiba baada ya kutoa heshima ya mwisho, mwili wake utapelekwa nyumbani kwake Kimara Temboni, baada ya misa takatifu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 atasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Julai 5, 2021.

Leave a Comment