×

Championi Gazeti Lagawa Jezi za Simba/Yanga Kwa Wasomaji Wake

Masoko wa Global Publishers, Samuel Eric (kulia) akimkabidhi jezi ya Timu ya Yanga msomaji wa Gazeti la Championi aliyekutwa akilisomo katika eneo la Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Global Publishers,Francis Johanes (kulia) akimkabidhi jezi ya Yanga msoamaji wa Gazeti la Championi.
Msomaji  wa Gazeti la Championi akionesha jezi ya Yanga aliyokabidhiwa baada ya kukutwa akilisoma gazeti hilo. 
Msomaji wa Gazeti la Championi akionesha jezi ya Yanga aliyokabidhiwa baada ya kukutwa akilisoma gazeti hilo.  Shabiki huyo alikuwa akisubiri nje ya Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Samuel Eric (kulia) akizungumza jambo na msomaji wa Gazeti la Championi aliyekutwa kwenye baiskeli aina ya Guta akilisomo wakati akielekea Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya Simba na Yanga.
Maofisa masoko wa Global wakiendelea na zoezi la kukabidhi zawadi.

Wadau wa Gazeti la Championi wakionesha mapenzi yao ya kulifuarahia gazeti hilo.

 

Mapema leo Timu ya Maofisa Masoko wametembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wasomaji waliokutwa wakisoma Gazeti la Championi ikiwa ni mahususi kwa kuwapatia zawadi za jezi mashabiki wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga unaochezwa leo Jumamosi Julai 3,2021.

Mashabiki hao walijinyakulia jezi hizo baada ya kukuta wasomaji hao wakiwa wamelinunua Gazeti la Championi ambapo pia Ofisa Masoko wa Global, Samuel Eric alisema:

“Lengo letu ni kuimarisha uhusiano kati yetu na mashabiki wa soka ambao ndiyo wadau wakubwa wa Gazeti la Championi, tutaendelea kugawa zawadi mbalimbali kutoka magazeti yetu.

 

 

Leave a Comment