×

Rais Samia Atua Uwanja wa Mkapa – Simba vs Yanga

Rais Samia Suluhu Hassan, akiangalia mpambano kati ya Watani wa Jadi Simba na Yanga unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Julai,2021.

Rais Samia leo Julai 3, 2021 mefika Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Yanga.

Rais Samia aliwasili majira ya Saa 10:57 jioni ikiwa ni dakika moja kabla timu hazijaingia Uwanjani kwa mchezo.

Rais Samia Suluhu Hassan, akiingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo tarehe 03 Julai, 2021 kwa ajili kuangalia mpambano kati ya Watani wa Jadi Simba na Yanga.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kuhudhuria mechi ya Ligi Kuu Bara tangu awe Rais wa Awamu ya sita.
Mara baada ya kuwasili Rais Samia alikwenda moja kwa moja juu kuketi huku maelfu ya mashabiki wa timu zote wakimshangilia kwa kelele sambamba na kumpigia makofi.

Rais Samia amepokelewa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallece Karia akiwa amekaa naye pamoja katika eneo la wageni maalum.

Leave a Comment