×

Kocha Simba Abadili Watatu, Nabi Sita

MBALI na Benchi la Ufundi la Yanga katika mchezo wa jana dhidi ya Simba kuwa na mabadiliko, pia upande wa wachezaji napo kulikuwa na mabadiliko makubwa tofauti na awali.

 

Kwa sasa Yanga ipo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye alichukua mikoba ya Cedric Kaze aliyekuwepo mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya 1-1.

 

Yanga ambayo katika mchezo wa Novemba 7, 2020 ilikuwa mwenyeji, ilianza na kikosi hiki; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong, Ditram Nchimbi na Farid Mussa.

 

Katika kikosi chao cha jana, kulikuwa na mabadiliko ya wachezaji sita ambao hawakuanza mchezo wa Novemba 7.

 

Waliokosekana ni Metacha ambaye amesimamishwa mechi tatu kutokana na tatizo la nidhamu na Lamine ambaye naye ana matatizo ya kinidhamu. Wengine ni Mustapha na Sarpong ambao ni majeruhi, huku Farid na Nchimbi wakianzia benchi.

Waliochukua nafasi zao ni Farouk Shikalo, Dickson Job, Zawad Mauya, Adeyum Saleh, Deus Kaseke na Yacouba Songne.Kikosi cha Yanga jana kilianza hivi; Farouk Shikalo, Kibwana Shomary, Adeyum Saleh, Dickson Job, Bakari Mwamnyento, Mukoko Tonombe, Zawad Mauya, Tuisila Kisinda, Deus Kaseke, Feisal Salum na Yacouba Songne.

 

Kwa upande wa Simba ambao jana walikuwa wenyeji, benchi lao la ufundi nalo lina marekebisho ambapo awali kocha alikuwa Sven Vandenbroeck, lakini sasa yupo Didier Gomes.

 

Kikosi cha Novemba 7 kilianza hivi; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, John Bocco, Clatous Chama na Luis Miquissone.

 

Chini ya Gomes, mabadiliko katika kikosi cha kwanza yapo matatu, waliokosekana ni Mkude, Bwalya na Mzamiru, huku maingizo mapya ni Bernard Morrison, Erasto Nyoni na Taddeo Lwanga.

 

Kikosi cha Simba jana kilianza hivi; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Taddeo Lwanga, Bernard Morrison, Erasto Nyoni, John Bocco, Clatous Chama na Luis Miquissone.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA,Dar es Salaam

Leave a Comment