×

Huku Kiba na Mondi, Kule Zuchu na Harmo

SOKO la Bongo Fleva linazidi kukua na hii inasababishwa na ukweli kwamba wasanii wanatoa nyimbo nyingi na nzuri ambazo zinavutia mashabiki.

 

Wiki iliyopita mambo yamekuwa ni mengi kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania baada ya wasaniii wakubwa kama Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kukabana koo na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ huku Zuhura Othman ‘Zuchu’ naye akikimbizana na Konde Boy, Rajab Abdul ‘Harmonize’.

KIBA VS MONDI

Wimbo ulitoka Juni 24, mwaka huu wa Saluti kutoka kwa Kiba akishirikiana na Rudeboy wa Nigeria, umeendelea kukimbizana na ule wa Kamata kutoka kwa Diamond au Mondi.

 

Katika Wimbo wa Saluti, Kiba anampa asante mpenzi wake ambaye alikuwa naye kwenye shida na sasa anamwambia shukran kwa kuweza kumvumilia.

 

Kwa upande wake Mondi, baada ya ukimya wa miezi saba, Juni 25, mwaka huu, alivunja ukimya kwa kuachia wimbo wake wa kwanza mwaka huu wa Kamata.

 

Wimbo wa Kamata ni mchanganyiko wa Afro-Pop na Bongo Fleva ambapo hadi jana ulikuwa kileleni kwenye mitandao mbalimbali ya muziki.

HARMO VS ZUCHU

Wakati Kiba na Mondi wakipambania kombe, ligi nyingine ilikuwa ni kati ya Harmonize au Harmo akiwa na wimbo wake wa Sandakalawe na mtoto wa Kizanzibar, Zuchu akikiwasha na Nyumba Ndogo.

 

Kwenye Sandakalawe, Harmo ametumia vionjo vya ladha mpya ya muziki ya Amapiano na kupitia wimbo huu ameonesha kuwa yeye anaweza kubadilika kwa kuimba mitindo tofautitofauti ya muziki.

Kwa upande wake, Zuchu amewashika mabinti wa mjini na Nyumba Ndogo ambapo imekuwa ni wimbo wa Taifa ambapo kwa spidi yake, hadi mwishoni mwa wiki jana video yake ilikuwa imeificha vilivyo ile ya Sandakalawe ambazo zilitoka kwa pamoja huku zikipishana saa moja pekee. Wenyewe wanasema ukikaa

Stori: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave a Comment