
MJADALA mkubwa umeibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya video mpya ya Harmonize, Sandakalawe kupata views milioni 4 ndani ya siku tatu huku akiwaacha mbali mastaa wenzake kama Diamond, Kiba na Zuchu ambao nao wameachia ngoma zao wiki iliyopita.
Licha ya kupata views wengi kiasi hicho ndani ya muda mfupi, lakini bado video ya Harmonize haijaweza kuzishusha ngoma ya Zuchu, ya Mondi na Kiba kwenye trending list ya YouTube, maswali yakaibuka kwa nini ama views nyingi lakini hajaingia trending number 1?
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Global Publishers ambaye ni mtaalam wa masuala ya digital contents, Edwin Lindege @eddynevo ameeleza kinaga ubaga kuhusu kilichotokea.
FULL VIDEO IPO YOUTUBE CHANNEL YA GLOBAL TV ONLINE