Kachero mmoja kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya maarufu kwa jina la Shiru, amepoteza fahamu kisha kufariki dunia akiwa kwenye sherehe ya kumuaga mwenzake (send-off).
Shiru alikuwa amegonga vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuwa kwenye ndoa na maofisa wawili wa ngazi ya chini.
Kwa mujibu wa rafiki zake, kifo chake kimezua maswali kibao kwa sababu hakuwa mgonjwa.
Kwa mujibu wa Televisheni ya K24, Shiru au Wanjiru alikuwa akihudhuria sherehe ya mwenzake katika eneo la Upper Hill siku ya Jumamosi iliyopita muda wa saa kumi na moja jioni ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Nairobi kabla ya kuthibitishwa kuaga dunia.
Rafiki zake walipokea taarifa za huzuni baada ya kuarifiwa kuwa kachero huyo alikuwa amefariki dunia hivyo mwili wake kuwekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Kisa hicho kimetokea miezi michache tu baada ya kachero huyo kugonga vyombo vya habari kutokana na kesi yake mahakamani.
Cc: @sifaelpaul
