×

Uingereza Kuondoa Vizuizi vya Corona

WAZIRI MKUU wa Uingereza Boris Johnson  ,  ametangaza hatua ya kuondoa vizuizi vya kudhibiti kusambaa virusi vya Corona, vya uvaaji wa lazima wa barakoa pamoja na kukaa umbali wa mita kadhaa Ifikapo Julai 19, 2021.

 

Vizuizi hivyo vitaondolewa katika kipindi cha wiki mbili zijazo licha ya kiwango cha maambukizo ya virusi hivyo kuongezeka kutokana na kusambaa kwa aina mpya ya kirusi cha Delta.

 

Waziri mkuu huyo wa Uingereza amesema ataweka wazi kuhusu namna ya nchi hiyo itakavyoweza  kuishi na virusi hivyo.

Hatua hiyo ya Johnson ni tafauti kabisa na mtazamo aliokuwa nao mwanzoni wa kuitazama Covid-19 kama adui anayetakiwa kuangamizwa.

hatua hizo mpya ni pamoja na uvaaji wa barakoa utakuwa wa hiari ispokuwa hospitali, baa pamoja na klabu za usiku zitafunguliwa, pamoja kukaa umbali wa mita moja maarufu kama Social Distance haitakuwepo.

 

Kiongozi huyo wa Uingereza ameashiria kwamba hatua za lazima za kudhibiti kusambaa virusi vya Corona zitaondolewa na watu watakuwa na hiari ya kufuata wanachotaka baada ya Julai 19.

Leave a Comment