
ASKOFU Dkt, Fredrick shoo, ambaye ni Mkuu wa KKKT, amechaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuwa Mwenyekiti.
Askofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian nchini Tanzania amempongeza Askofu. Dk Shoo kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo kwa kumuandikia kwenye kurasa zake za kijamii;
“Ninampongeza Mhashamu Baba Askofu Dk Fredrick Shoo kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
“Kuchaguliwa kwa Dk. Shoo ni dalili nzuri kwa CCT katika kuimarisha misingi na madhumuni ya kuanzishwa kwake.
“Nikiwa mtu ambaye niliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo, ninaelewa umuhimu wa mtu kama Dkt. Shoo kuiongoza Jumuiya hiyo katika mazingira ya sasa! Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!”
Askofu Dk. Shoo anatambulika kwa misimamo yake mikali katika kutetea na kupigania haki, uhuru na utu wa wananchi bilia kujali tofauti za kidini na kisasa.
“Askofu Dkt. Shoo pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Moshi.