




Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo Julai 09, 2021 amewapokea na kuwakubali Mawakili wapya wa Kujitegemea 308 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Idadi hii ya Mawakili wapya wa kujitegemea inaongeza idadi na kuwa na jumla ya Mawakili wa Kujitegemea 10,436 nchini.