VIDEO ya askari wa usalama barabarani katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, akiibiwa siku yake ya mkononi na wanaume watatu waliokuwa kwenye pikipiki imetrendi sana kwenye mitandao ya kijami wiki hii.
Picha ya video hiyo iliyorekodiwa na dashcam, sinamuonesha afisa huyo akizungumza kwa simu yake kabla ya mwendesha pikipiki kupita na abiria ambaye alinyakua simu kutoka kwa polisi.
Wanaume hao wawili walitoweka kwenye msururu wa magari na kumuacha polisi akionekana hana la kufanya. Haijawa wazi ni wapi hasa video ya tukio hilo ilichukuliwa ,lakini video inaonesha ilichukuliwa mwezi wa Julai.
Uporaji wa simu za mkononi, mikoba na vipuli unaofanywa na wezi wanaotumia pikipiki umekithiri jijini Nairobi. Maafisa wamekuwa wakiwaonya watu kuwa macho wakati wanapotembea kwenye mitaa ya jiji la Nairobi.
Uhalifu kama vile ujambazi na utekaji nyarapia umeongezeka huku polisi wiki hii wakitangaza kuunda kikosi maalum cha kukabiliana na uhalifu huu.
