RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kuanzia leo Julai 16-17 kwa mwaliko wa Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.
Katika hotoba yake Rais Samia amesema Moja ya lengo la kwenda Burundi ni kujitambulisha baada ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa rais , Hayati Dkt. Magufuli, “ukiwa mgeni kwenye mtaa lazima ujitambulishe, napita kujitambulisha kwa wenzangu Afrika Mashariki.”
Aidha Rais Samia ameongeza kuwa Safari yake hiyo niya kuimarisha urafiki na undugu uliopo baina ya mataifa hayo mawili ambao ni enzi na enzi.
Nimekuja Burundi kwa lengo la kukuza na kuimarisha urafiki zaidi, udugu na ujirani uliopo kwa mataifa yetu. Tunao uhusiano si tu wa kirafiki bali wa damu kwa enzi na enzi. Nimekuja kuzungumza na Rais Ndayishimiye ili kujadili namna ya kuendeleza uhusiano huo.”
Pia ameweka wazi kuwa amefanya mazungungunzo ya kina na Rais Ndayishimiye namna ya kukuza biashara kati ya Tanzania na Burundi imeongezeka kutoka Sh. Bil. 83.9 mwaka 2015 hadi Sh. Bil. 200.1 mwaka 2019.
“Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimesajili miradi 18 ya Burundi yenye thamani ya dola za Marekani mil 2019.4 ambayo imetoa ajira 3,544 ukiwemo mradi wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom wenye thamani ya dola mil 180.”
Pia Serikali zote mbili zimekubaliana kushirikiana kuboresha mazingira ya biashara ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya kodi na visivyo vya kodi, ikiwemo kuharakisha ujenzi wa kituo cha pamoja katika mpaka wa Manyovu Mgina.
“Tumekubalaiana kujenga Barabara zinazounganisha nchi zetu mbili ikiwemo Nyakanazi, Kasulu, Manyovu na Gitaza. Tumekubaliana kujenga reli ya Uvinza, Msongaji, Gitega. Tumewaelekeza mawaziri wetu kutafuta fedha kuharakisha ujenzi wa reli hiyo” ameongeza Rais Samia.
