Vodacom Yashinda Tuzo ya Kampuni Bora ya Mawasiliano
Global Publishers July 16, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Meneja wa maduka ya rejareja wa Vodacom Tanzania Plc Vanessa Mlawi akionyesha tuzo baada ya kampuni hiyo kushinda kwenye maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam. Vodacom Tanzania ilishinda tuzo hiyo baada ya kuwa kinara kutokana na huduma bora zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye maonesho kupitia kundi la sekta ya mawasiliano.
Kampuni ya Mawasiliano Vodacom imeshinda Tuzo ya Kampuni Bora ya Mawasiliano kwenye maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam. Vodacom Tanzania ilishinda tuzo hiyo baada ya kuwa kinara kutokana na huduma bora zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa kupitia kundi la sekta ya mawasiliano.