×

Mwanamke Mwenye Kucha Ndefu Zaidi Duniani

AYANNA Williams, mwanamke anayeishi Texas nchini Marekani, ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya Kitabu cha Kumbukumbu cha Guinness World Records ya kuwa na kucha ndefu zaidi duniani, lakini hatimaye amezikata baada ya miaka 30.

 

Kwa mujibu wa Guinness World Records, Ayanna aliweka rekodi yake ya kwanza baada ya kucha zake kuwa na futi 24 kabla ya kuzikata wiki iliyopita.

 

Ayanna aliweka rekodi hiyo tangu mwaka 2017 ambapo kucha zake zilikuwa zina futi 18 na alikuwa anatumia chupa mbili za rangi kwa ajili ya kuziremba.

 

“Nimekuwa nikizifuga kucha zangu kwa miongo kadhaa hadi sasa, Lakini sasa niko tayari kwa maisha mapya, najua nitazimisi sana, lakini wakati wa kuzitoa ndiyo umefika.

 

Ayanna alisema kuwa, alikuwa anashindwa kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kuosha vyombo, kufua nguo na kutandika kitanda kwa sababu ya kucha zake hizo ndefu.

 

“Bado nitasalia kuwa Malkia wa Kucha nikiwa nazo au la, Allison Readinger wa Trinity Vista Dermatology mjini Forth Worth jijini Texas ndiye alimkata Ayanna kucha hizo akitumia kifaa cha elektroniki.

 

Video ya dakika 8 inayomuonesha Allison akikata kucha za Ayanna iliyochapishwa kwenye Mtandao wa YouTube imeendelea kuwa gumzo kwa wengi, Ayanna ambaye alikulia katika Jimbo la Texas, amekuwa akizipenda mno kucha zake na kuziremba.

Ayanna aliwaambia Guinness World Records namna ambavyo alikuwa akimuomba mama yake kukagua urefu wa kucha zake kila mara na kuzifurahia.

 

“Na shughuli zangu lazima niwe mwangalifu sana. Kwa hiyo kwenye akili yangu nilikuwa najaribu kuchukua tahadhari kubwa mno katika hatua yangu nyingine ili kuhakikisha sijiumizi na kucha zangu au kuzivunja,” alisema Ayanna.

 

Ayanna anasema kuwa, kwa sasa anafurahia kukata kucha zake na kufungua ukurasa mpya wa maisha yake.

Anasema kuwa, anaazimia kufuga kucha zake hadi inchi sita pekee, kulingana na Ripley, kucha zake alizokata zitawekwa katika kumbukumbu mjini Orlando, Florida.

Sifael Paul

Leave a Comment