
KAMPUNI ya simu Infinix imewataka wateja wa simu za Infinix kuendelea kutembelea maduka yao na kukaa karibu na kurasa ya @infinixmobiletz ambapo Infinix itawatangaza rasmi washindi watakaozawadiwa Music system. Infinix ilizindua rasmi promosheni ya NOTE 10 Big Mnyama na kwa kila mteja aliyenunua au atayenunua simu ya Infinix NOTE 10 basi kuzawadiwa Blenda, jagi la umeme, wireless earphone papohapo.
Infinix kuhitimisha promosheni hii ya NOTE 10 Big Mnyama jumamosi hii kwa kuchezesha droo kubwa ya bahati itakayohusisha wateja wa NOTE 10 na mshindi kuondoka na Music System pamoja na blenda lakini pia kwa siku hii Infinix NOTE 10 itapatikana kwa bei punguzo badala ya kulipia 530,000Tsh utaipata kwa sh. 430,000 na NOTE 10 pro utaipata kwa sh.550,000 badala ya kulipia sh.700,000.
Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro zilizinduliwa mapema mwezi Mei nchini Tanzania na sifa kuu ya simu hizi ni ufanisi wa G95 processor na kamera ya MP64 na teknolojiaya 4K video resolution ambayo ndio teknolojia bora kwasasa katika kutengeneza filamu.

Kampuni ya simu Infinix imejidhatiti katika uzalishaji wa simu zenye ubora, huduma bora kwa bei rafiki ili kuongeza matumizi ya kidijitali kujifunza mambo mengi kwa muda mfupi.
Tembelea jumamosi hii maduka ya simu kariakoo upate NOTE 10 na NOTE 10 pro kwa punguzo la bei.