×

Breaking News: Mbowe Afikishwa Mahakamani

 

MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anadaiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya ugaidi yanayomkabili leo Jumatatu, Julai 26, 2021.

 

CHADEMA kimedai kuwa Mbowe alifikishwa mahakamani kimyakimya na kusomewa mashtaka ya ugaidi kisha kupelekwa gerezani. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, inadai kuwa taarifa zaidi kuhusu sakata hilo, zitatolewa baadaye na chama hicho.

 

Kiongozi huyo wa chama hicho, kikuu cha upinzani nchini, alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia kwa ajili ya kushiriki kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

 

Hata hivyo, siku iliyofuata Msemaji wa Polisi nchini, David Misime aliueleza umma kuwa Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

 

Katika taarifa iliyotolewa leo Julai 26, 2021 na Mkurugenzi wa Itifaki Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema imesema kuwa awali mawakili na familia yake waliambiwa Mbowe anapelekwa hospitali, lakini akapelekwa mahakamani, akasomewa mashtaka na kurudishwa mahabusu.
 

Leave a Comment