×

Shabiki Simba Avuliwa Nguo Zote

ALMANUSRA atolewe roho jamaa mmoja aliyetambulika kwa jina la Juma aliyedaiwa kuwa ni shabiki wa Simba baada ya kutokea uwanjani wakati Yanga wakiwa wanajiandaa kwenda kukagua uwanja.

 

Shabiki huyo ambaye alikuwa amevalia jezi ya Simba alijikuta akivamiwa na makomando wa Yanga na kupokea kichapo bila kupewa muda wa kuzungumza huku makomando hao wakimhoji amefuata nini.

 

Kichapo kiliendelea mfululizo huku akivuliwa nguo na kuachwa na bukta ya ndani na hakupata msaada wowote kwani asilimia 100 uwanja ulikuwa umezungukwa na watu wa Yanga.

 

Kilichomnusuru Juma ni kupungua kwa hasira za mashabiki hao ambao baada ya kuona jamaa hajiwezi wakaamua kumuacha. Tukio hilo lilijiri jioni ya juzi Jumamosi saa chache kabla ya mchezo kuanza.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

 

Leave a Comment