×

Waziri Ummy Apiga Marufuku Matumizi ya ‘Fedha Mbichi’

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amepiga marufuku kwa matumizi ya fedha ambazo zimekusanywa na Halmashauri na hazijapelekwa benki kwa sababu yoyote huku akiwataka wakurugenzi wanahakikisha wanasimamia hilo.

 

Waziri Ummy amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari leo, wakati akitoa taarifa za makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo ametaka fedha zikikusanywa kupeleka benki ndo zitumike.

 

“Nielekeze Halmashauri kuhakikisha fedha za makusanyo ya ndani zinazokusanywa zinapelekwa benki ndani ya masaa 24 baada ya kuzikusanya ni marufuku na kosa kisheria kwa halmashauri kutumia fedha zilizokusanywa kabla ya kuzipeleka benki (Fedha mbichi),” amesema Waziri Ummy.

 

“Wakuu wa idara na wakurugenzi ni marufuku kuchukua fedha mbichi amabazo zimekusanywa na hazijapelekwa benki hata kama kuna dharura yeyote, fedha zipelekwe benki ndo zitumike, benki unaweka hela na unatoa siku hiyohiyo” alisisitiza Waziri Ummy.

 

Aidha, Waziri Ummy amezitika Halmashauri zote nchini kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kusubiria fedha kutoka serikali kuu.

 

“Nitaishangaa halmashauri amabyo itashindwa kujenga hata nyumba moja ya mwalimu kwa mwaka kwasabhu tumeoeleka walimu vijijini changamoto kuuni nyumba ni nataka halamashauri sasa hivi nazo zijenge nyumba za walimu na taraifa zetu inaonyesha mil 50 unajega nyumba ya kuweka kaya mbili za walimu,” amesema Ummy.

 

Waziri Ummy ametoa taraifa ya makusanyo nakuzitaja Halmashauri zilizongoza kwa kukusanya mapato mengi kuwa ni Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam sh. Bil.67.09, ikifuatiwa na Manispaa ya Kinondoni Bil 40.7 na Halmashauri ya Dodoma Bil.38.4 huku Halmashauri 9 zikiwa zimekusanya chini ya Bil 1.

Leave a Comment