×

Mjane wa Kapteni John Komba, Azindua Ukumbi wa Kisasa Dar

Mama Salome Komba akizungumza kwenye uzinduzi wa ukumbi huo.

 

 

MJANE wa aliyekuwa kiongozi wa Kundi la ToT, Hayati John Komba, Bi Salome Komba baada ya kifo cha memewe sasa ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali kwa kushughulisha na mambo mbalimbali ambapo wikiendi iliyopita amezindua ukumbi wa kisasa kabisa ambao ni kwa ajili ya sherehe na mikutano mbalimbali.

Biharusi mtarajiwa Glory akijiandaa kukata keki kwenye Send- Off ambayo ni ya kwanza ukumbini hapo.

 

 

Akizungumza na wanahabari wetu Mama Salome Komba amesema aliamua kujenga ukumbi wa kisasa unaoitwa Salome Social Hall kama kumbukumbu ya mumewe ambaye alimshauri kufanya hivyo siku chache kabla ya kifo chake.

Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio.

 

 

Akiuelezea ukumbi huo uliopo Mbezi Tangi Bovu kwenye kituo cha daladala cha Kwa Komba, Mama Salome amewakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo waliokuwa mashabiki wa marehemu mumewe kumuendi kwa kwenda kukodi ukumbi huo.

Mambo yakiendelea.

 

 

Amesema kwa wanaohitaji kupatiwa huduma ya mapambo, keki, vinywaji na vya vyakula vyote vinapatikana ukumbini hapo.

Mama Salome akihojiwa na Mwandishi wa Global Tv na +255Global Radio, Zari The Boss.

 

 

“Nimeona nijiongeze maana nitakaa chini na kujiita mjane mpaka lini na pia sehemu ya mapato ninayopata kwenye biashara hii naitumia kwenda kuwasaidia wajane wenzangu, watu wenye uhitaji maalum na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali.

 

 

Nawaomba na wajane wenzangu waache kukaa chini na kuendelea kujiita wajane wapambane katika ujasiriamali ili maisha mengine yaendelee”, amesema Mama Salome.

 

 

Mama Salome amewataka wadau wanaotaka kumuunga mkono kwenye ukumbi huo kutumia namba ya mawasiliano 0752345234 au kufika eneo hilo.

Leave a Comment