Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja UBA Tanzania Dora Kyungu akimsikiliza kwa makini mmoja wa mteja wa benki hiyo wakati wa kuadhimisha miaka mitano ya falsafa ya mteja kwanza. Falsafa ya ‘Mteja Kwanza’ ni mpango uliozinduliwa Mwaka 2016 ukiwa na lengo la kuifanya Benki iwe na uelekeo na mtazamo kwa wateja.
Dar es Salaam Jumanne 3 Agosti 2021… Falsafa ya ‘Mteja Kwanza’ ni mpango uliozinduliwa Mwaka 2016 ukiwa na lengo la kuifanya Benki iwe na uelekeo na mtazamo kwa wateja.
Hii ikibeba maana kubwa sana ya kuwaelewa wateja na kuyaweka mbele na kuyachukulia kwa uzito Mkubwa mahitaji yao hasa katika kila tunachofanya katika huduma zetu za kila siku.
Falsafa hii pia inatumika katika bidhaa na huduma bunifu na zilizoboreshwa zinazotolewa na Benki yetu ambazo hulenga katika kumfanya mteja afaidike na kumuinua kimaisha.
Pamoja na haya, wiki iliyopita Benki ya UBA ilifanya maadhimisho ya miaka mitano ya Mteja ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa UBA, Bw Kingsley Ulinfun alionesha kwa vitendo kwa kuwakaribisha wafanyakazi wote walipokuwa wanaanza siku mpya ya kazi lakini pia kutumia muda wao kuwasikiliza na kuwahudumia wateja, ikiwa inaonesha ni jinsi gani benki inajitoa kuwahudumia na kuwathamini wateja wake.
Kukuwa na ongezeko Kubwa na Miamala ya kielekroniki, Benki ya UBA imetengeneza kituo chenye uwezo Mkubwa (Omni channel) ili kufuatilia kwa karibu malipo na miamala mingi hivyo kuweza kuboresha kwa kiasi kikubwa huduma kwa wateja.
Pia wateja wamepewa fursa ya kuweza kuperuzi akaunti zao popote na Wakati wowote wakitumia huduma bora kabisa za Benki ya UBA. Huduma hii pia inapatikana kupitia simu Janja, kompiuta, kompiuta mpakato na vifaa vingine vyote vinavyoweza kutumia huduma ya intaneti.
Leo Benki ya UBA inatarajia kutengeneza mara moja majibu na maazimio juu ya malalamiko ya wateja, usimamizi wa uhusiano bora kati ya viongozi na wa wateja, mawasiliano makini na salama kwa wateja juu ya bidhaa na huduma za Benki
Maendeleo na ukuaji wa wateja ni sehemu muhimu sana katika mikakati ya Benki yetu.
Tunajizatiti katika kuyaishi na kwenda mbele zaidi katika kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.