×

Miquissone Anasepa, Simba, Al Ahly Wamalizana

TETESI: KLABU ya Simba imekubali ofa ya dola za Marekani 900,000 (zaidi ya Tsh Bilioni 2) kumuuza mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa Mabingwa wa Afrika, Klabu ya Al Ahly ya Misri.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tayari Simba na Ahly wamefikia makubaliano hayo ambapo Miquissone amekubali kujiunga na Al Ahly kwa mkataba wa miaka minne.

Leave a Comment